Swali: Ni ipi maana ya maneno yetu pale tunaposema katika du´aa yetu ya kufungulia swalah:

وتعالى جدك

“Utukufu Wako uko juu.”?

Jibu: Maana yake ni kwamba ukuu na utukufu Wako uko juuu. Amesema (Subhaanah) katika Suurah “al-Jinn” juu ya majini ya kwamba walisema:

وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا

“Na kwamba hakika umetukuka kabisa utukufu wa Mola wetu, hakujifanyia mke wala mwana.”[1]

[1] 72:03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/74)
  • Imechapishwa: 11/01/2022