Haya wanayodai – yaani Mufawwidhwah – ni kosa. Maana ya kulingana na maana ya sifa za Allaah inajulikana. Namna yake ndio haijulikani. Maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

Kulingana ina maana zifuatazo:

1 – Kutulia/kuthibiti (استقر).

2 – Kuwa juu (علا).

3 – Kuwa juu (ارتفع).

4 – Kungatika (صعد).

Hizi ndio maana nne za kulingana (الاستواء) katika lugha ya kiarabu. Hata hivyo hatujui namna Allaah alivyolingana juu ya ´Arshi. Hivyo ndivyo alivyosema Imaam Maalik alipoulizwa maana ya kulingana ambapo akajibu kwa kusema:

“Kulingana kunajulikana.”

Yaani maana yake inajulikana katika lugha ya kiarabu.

  • Mhusika: ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah, uk. 20
  • Imechapishwa: 01/05/2020