Maamuma kumkumbusha imamu kwa kumwambia afanye kadhaa

Swali: Kuna Imamu amefanya makosa na akasahau Rakaa moja. Mmoja katika maamuma akazungumza na kusema “Zidisha Rakaa, ewe Imamu”. Ni ipi hukumu ya Swalah ya maamuma huyu?

Jibu: Ikiwa amefanya hivo kwa kukusudia, Swalah yake inabatilika. Ama ikiwa ni mjinga au amesahau na akazungumza, Swalah yake ni sahihi – in shaa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (73) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14115
  • Imechapishwa: 17/11/2014