Swali: Maafikiano (الإجماع) ni hoja ya kukata kabisa au ya dhana?

Jibu: Maafikiano yenye yakini ni hoja ya kukata kabisa. Ni moja katika ile misingi mitatu ambayo haijuzu kwenda kinyume nayo; Qur-aan, Sunnah sahihi na maafikiano.

Inapasa kujua kuwa maafikiano ya kukata yaliyokusudiwa ni yale maafikiano ya Salaf kutoka katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anhum). Kwa sababu baada yao tofauti zilikuwa nyingi na zikaenea katika ummah. Hayo yamezinduliwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” na wanazuoni wengine.

Miongoni mwa dalili za kwamba maafikiano ni hoja ya kukata kabisa ni maneno Yake (Ta´ala) katika “an-Nisaa´”:

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”[1]

[1] 04:115

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/427)
  • Imechapishwa: 11/07/2021