Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya bahari:

“Maji yake ni twahara na maiti yake ni halali.”

Inajumuisha mnyama maiti wa ndani ya mto?

Jibu: Midhali mnyama anaishi ndani ya maji peke yake ni katika maiti wa bahari. Ni mamoja inahusiana na mto au bahari. Midhali anaishi tu ndani ya maji ni halali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020