Lini waswaliji wanasimama kwa ajili ya swalah?

Swali: Je, kuna wakati maalum wa kusimama kwa ajili ya kuswali wakati wa kusikia Iqaamah? Kwa msemo mwingine ni kwamba asimame wakati anapomsikia muadhini akisema:

قد قامت الصلاة

“Swalah imesimama.”

au kabla yake au baada ya kumaliza kwake kukimu? Au pengine jambo ni lenye wasaa?

Jibu: Kusimama kwa ajili ya kuswali hakuna wakati maalum katika Shari´ah iliyotakasika. Bali inafaa kwa waswaliji kusimama kwa ajili ya kuswali mwanzoni mwa Iqaamah, katikati yake au mwishoni mwake. Jambo ni lenye wasaa. Sijui dalili ya ki-Shari´ah inayofanya wakati maalum wa waswaliji kusimama wakati wa kusikia Iqaamah. Wanazuoni waliosema kuwa imesuniwa kusimama wakati muadhini anaposema:

قد قامت الصلاة

“Swalah imesimama.”

sitambui dalili yao katika jambo hilo.

Lakini ikiwa wakati wa kukimu imamu hajahudhuria, basi Sunnah kwa waswaliji wasisimame mpaka wamuone. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapokimiwa kwa ajili ya swalah basi msisimame mpaka muone nimetoka.”

Ameipokea Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/367)
  • Imechapishwa: 24/09/2021