Lini mwanamke anatwaharika kutoka katika hedhi?

Swali: Kuna mwanamke anajiliwa na hedhi kwa muda wa siku saba na inakatika siku hiyohiyo ambapo anabaki siku ya nane na ya tisa na huku yuko na umanjano na uchafuchafu. Siku ya kumi ndipo anaona weupe. Afanye nini; aswali na afunge katika siku ya nane na ya tisa? Ni kipi kinachokusudiwa na kutwaharika; je, ni kule kukatika kwa damu au kukauka kwa damu, kitu kingine au kuonekana weupe?

Jibu: Makusudio ya kutwaharika na hedhi ni kukatika/kusita kwa damu na sio kukauka. Kwa sababu mwanamke hedhi yake wakati mwingine inaweza kukauka kwa siku moja au nusu ya siku, hii inazingatiwa ni hedhi. Lakini ikikatika na akatambua kuwa imekatika basi ametwaharika. Haijalishi kitu hata kama baada ya hapo ataona umanjano au uchafuchafu basi haidhuru. Umm ´Atwiyyah amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na uchafu baada ya kutwaharika kuwa ni kitu.”[1]

[1] Abu Daawuud (307).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1129
  • Imechapishwa: 12/06/2019