Lini inafaa kuwakilisha mtu amhijie mwenzake na ni lini haifai kufanya hivo?

Swali: Nina ndugu yangu mmoja aliye katika mji wa Kiislamu ambaye anataka kuniwakilisha nimfanyie hajj ilihali ni muweza wa kuifanya. Lakini hata hivyo nchi yake haimruhusu kwenda hajj kwa kuwa hajafikisha miaka ya hajj ambayo imepangwa na nchi hiyo. Nikamwambia kwamba nitakuuliza wewe kwanza hukumu ya masuala haya kisha nikweleze. Je, ni sahihi kumhijia?

Jibu: Mwambie kwamba si sahihi kwako kumuhijia. Kwa sababu kizuizi hiki kinatarajiwa kuondoka. Kitaondoka wakati atapofikisha miaka ya nidhamu zilizowekwa na nchi yao. Kikwazo ikiwa kinatarajiwa kuondoka basi haijuzu kwa yule ambaye anawajibika kuhiji kumuwakilisha mwingine.

Kwa ajili hii tunasema ukifika wakati wa hajj na mtu akapatwa na ugonjwa wa kawaida ambao unatarajiwa kupona, haifai kwake kuwakilisha mtu. Lakini ikiwa ni maradhi yenye kuendelea ambayo hayatarajiwi kupona inafaa kwake kuwakilisha mtu. Kwa hiyo amweleze rafiki yake kwamba hajj kwa sasa haimlazimu. Kwa sababu si muweza. Vilevile haijuzu akawakilisha mtu. Kwa sababu kikwazo chake kinatarajiwa kuondoka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/929
  • Imechapishwa: 25/11/2018