Swali: Kipindi cha nyuma kumeenea msemo unaosema ya kwamba Ashaa´irah na Maaturiydiyyah ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni ipi taaliki yako kwa msemo kama huu?

Jibu: Ni lini walikuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakati wanawafanyia uadui Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wanawanyanyasa kutokana na historia? Ni lini walikuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakati wanafasiri:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa Rahmah, Amelingana juu ya ´Arshi Yake.” (20:05)

ametawala na hawathibitishi kulingana, al-Istiwaa´?

Ni lini walikuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakati wanasema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa na maana yake inatoka kwa Allaah? Watu sampuli hii ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Kamwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 11/08/2020