Lingania kwa Allaah kwa upole na ulaini na epuka ukali na ususuwavu

Swali: Ni ipi njia sahihi ya kuwalingania watu katika dini ya Allaah? Ni zipi tutaweza kuziteka nyoyo za watu?

Jibu: Ulinganizi sahihi ni ule ambao Allaah (´Azza wa Jall) amemtajia Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.” (Ibraahiym 16:125)

Ni juu yako kulazimiana na upole. Kwani upole hauwi katika kitu isipokuwa hukipamba na hauuondoshwi kwenye kitu isipokuwa hukifanya kikawa kibaya. Allaah alimuusia Muusa na Haaruun (´alayhimaas-Salaam) wamwambia kiumbe muasi zaidi kwa Allaah maneno laini. Ni juu yako kufanya ulaini. Epuka ususuwavu. Subiri juu ya yale utayokutana nayo kutoka kwa nduguyo usipopata kutoka kwake kukubali kwa haraka. Lakini usikate tamaa. Bali kariri. Huenda kuongoka kukapatikana mara ya ishirini au zaidi ya hapo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1053
  • Imechapishwa: 27/05/2020