Lingania katika haki na usijali wakorofi


Swali: Kuna mlinganizi katika nchi yetu ambaye amekuwa maarufu kupitia mihadhara, kaseti na vyombo vya mawasiliano. Ana makosa katika Da´wah yake yanayoenda kinyume na Sunnah na ´Aqiydah. Wakati tunaporaddi upotevu wake kwa hoja na dalili, watu wanapinga na kusema analingania katika Uislamu na amefanya hili na lile. Kisha wanauliza ni nini tumeufanyia Uislamu na kwa nini tunamkosoa.

Jibu: Ni jukumu lenu kulingania katika dini ya Allaah. Msiwajali wasaliti na wakorofi. Msiwajali. Hamkuja kuwaridhisha watu. Mmekuja kumridhisha Allaah. Ikiwa mko katika haki na mnafuata njia ya haki mfumo sahihi, msiwajali wale wenye kuwapinga na kueneza uvumi juu yenu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu'
  • Imechapishwa: 05/09/2020