Lete dalili moja tu inayopinga waumini kumuona Allaah Aakhirah?


Ni wapi anaweza kutoa dalili moja tu yenye kuzingatiwa inayokanusha waumini kumuona Mola wao Aakhirah? Hana jengine isipokuwa utata, utatizi na udanganyifu wa kutaja dalili zinazokanusha kuonekana kwa Allaah hapa duniani na kutaka kufanya zionekane kuwa ni zenye kukanusha Allaah kuonekana duniani na Aakhirah. Utatizi wake utafichuka pindi atapotaja dalili za wenye kukanusha [kuonekana Allaah Aakhirah] kama anavyodai.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 89
  • Imechapishwa: 14/01/2017