Leo mke anaweza kujua mume atafika saa ngapi

Swali: Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mwanaume kurudi kwa familia yake usiku kutoka safarini ili kutazama kama wanamdanganya au kutafuta makosa yao.”[1]

Kuna wanaosema kuwa leo kutokana na spidi ya vyombo vya mawasiliano mke anaweza kujua ni lini mume wake atafika ili aweze kujiandaa kwa kufika kwake. Je, fikira hizi ni kupingana na Hadiyth?

Jibu: Hapana, sio kupingana na Hadiyth. Sababu, ya familia kutokujua juu ya kufika kwake na ujio wake wa kushtukiza imeondoka. Ama leo kutokana na vyombo vya mawasiliano watajua ni lini atafika nyumbani. Kwa njia hiyo makatazo yameondoka.

[1] Muslim (3566).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017