Lazima kuthibitisha kwa hakimu

Swali: Kuna mtu amepatwa na maradhi ya uchawi na akawa hajui anachokisema na matokeo yake akamtaliki mke wake zaidi ya mara ishirini kisha baadaye hali yake ikaboreka na hivi sasa anataka kumrejea. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Haya yanarejeshwa kwenye vyombo vya Shari´ah ili kuthibitisha wakati alipotoa talaka kweli alikuwa amepoteza fahamu. Jambo hili linarejea kwa hakimu ambaye atahoji kuhusu maudhui haya. Je, alikuwa na fahamu wakati wa kutoa talaka au hakuwa na fahamu? Ni lazima lithibitishwe jambo hili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/رجل-طلق-زوجته-عدة-طلقات-وهو-مسحور
  • Imechapishwa: 18/06/2022