Lazima kufululiza wakati wa kulipa deni la Ramadhaan?

Swali: Si sharti kufuatanisha wakati wa kulipa deni la Ramadhaan. Je, inafaa kwa mtu mara akafunga na mara akaacha na kadhalika?

Jibu: Ndio. Si sharti kufuatanisha. Afunge na kulipa kulingana na uwezo wake.  Lakini mtu akiweza kufuatanisha ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/421)
  • Imechapishwa: 17/03/2022