Swali: Mume anakataa kutoa mahari yaliyobaki pamoja na kuwa ni mwenye wepesi wa kufanya hivo pamoja na kwamba alikubaliana na walii wa mwanamke kwamba ni moja ya mambo mawili: kifo au talaka. Mke anayahitajia sana. Ni ipi hukumu?

Jibu: Hukumu ni kwamba katika nafasi hii sharti ndio yenye nguvu zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waislamu wako kwa mujibu wa masharti waliowekeana.”

Midhali mume alishurutisha kuchelewesha mahari katika moja ya mambo mawili; ima kifo au kutengana, basi yuko kwa mujibu wa yale aliyoshurutishiwa. Uhakika wa mambo ni kwamba lawama zinamwendea mwanamke na yule msimamizi wake aliyemuozesha. Lililokuwa la wajibu kwa mwanamke alitakiwa kuikataa sharti hii wakati wa kufunga ndoa. Walii wa mwanamke endapo alitaka kuweka sharti hii basi alitakiwa kumshauri mwanamke kwanza. Kwa sababu mahari sio haki ya baba, kaka wala ami. Mahari ni haki ya mwanamke. Amesema (Ta´ala):

وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً

“wapeni wanawake mahari zao kwa raha zao.” (04:04)

Mwanamke huyu anatakiwa kuwa na subira na kuvuta subira. Mume akiweza kutoa hichi kilichobaki bila shaka ni kheri. Asipoweza au akaweza lakini akakataa kutoa kutokana na sharti hii waliowekeana, basi jambo liko kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/798
  • Imechapishwa: 22/01/2018