Swali: Nimesikia jibu lako kuhusu ulinganizi wenye kupangwa na makundi ya mashirika. Nimeshakusikia hapo kabla ukizungumzia kuhusu makundi na kuwa kila kundi linatakiwa lifanye kazi mahala pake. Kipindi cha nyuma nimekusikia ukikemea ukundi-ukundi na mambo ya mashirika. Vipi tunaweza kufahamu yote haya?
Jibu: Hakuna mgongano. Hivi sasa sisi tumekaa kwenye kikao kilichopangwa. Tumepangwa na wakati huo huo tunakemea mashirika. Mashirika tunayokemea ni yale ambayo watu hujiwekaemo ili kutangaza nchi ya Kiislamu kwenye usiku mmoja. Mashirika kama haya yameundwa kwenye mashirika ambayo yanajulikana kati ya Waislamu. Inahusiana kwa mfano na mashirika ya kisiri, maandalizi ya kimali, kuunda nchi ndani ya nchi nyingine, kuunda kamji kadogo ndani ya nchi nyinginezo na mfano wa haya. Ni mashirika kama haya ndio ambayo wengi katika watu wa makundi makundi hujiunga ndani yake ambayo tunakemea.

Ama kuhusiana na mashirika yanayofundisha, nasaha, kuamrisha mema, kukataza maovu na mambo mengine ambayo Uislamu umeweka, hatuyakemei.

Kwa kifupi tunakemea mashirika yanayoleta ukundi-ukundi, lakini hatukemei mashirika ambayo hayaleti ukundi-ukundi unaotenganisha Ummah katika makundi na mapote. Hakuna anayeweza kukataza shirika linalowafundisha watu Uislamu wa haki. Pengine umeona kuwa hakuna mgongano kwa yale niliyosema.

Swali: Nijuavyo ni kuwa makundi haya yamejifanya vyama-vyama.

Jibu: Mimi sikuzungumzia kuhusu kundi maalum na kama limewekwa katika Shari´ah au hapana. Ninasema kuwa kundi lolote lililojiweka vyama-vyama na shirika linalotoa bay´ah kwa kiongozi na mfano wa hayo husababisha tu Waislamu kufarikiana na kutofautiana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (27)