Latwiyf ni jina la Allaah?

Swali: Je, Latwiyf ni katika Majina ya Allaah (´Azza wa Jalla)?

Jibu: Bila ya shaka Latwiyf ni katika Majina ya Allaah (´Azza wa Jalla):

وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ

“Naye ni Al-Latwiyful-Khabiyr (Mwenye kudabiri mambo kwa utuvu – Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).” (06:103)

اللَّـهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ

“Allaah ni Latwiyfun (Mwenye kudabiri mambo kwa utuvu) kwa waja Wake.” (42:19)

وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ

“Na hali Yeye ni Al-Latwiyful-Khabiyr (Mwenye kudabiri mambo kwa utuvu – Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).” (67:14)

 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-6-2.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014