Laana kwa mke inazingatiwa ni talaka?


Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kuwalaani baadhi ya wakeze au watoto wake? Je, laana inazingatiwa kuwa ni talaka?

Jibu: Haijuzu kumlaani mtu. Hakuzingatiwi kuwa ni talaka. Bado ni mwenye kuendelea katika usimamizi wake. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah kutokamana na hilo na amwombe msamaha kwa kule kumtukana. Kadhalika haijuzu kuwalaani wanawe na wengineo katika waislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kumtukana muislamu ni dhambi nzito na kumuua ni ukafiri.”[1]

“Kumlaani muumini ni kama kumuua.”[2]

Hadiyth hizi mbili Swahiyh zinajulisha kwamba mtu kumlaani ndugu yake muislamu ni dhambi kubwa. Kwa hivyo ni lazima kutahadhari hilo na mtu achunge mdomo wake kutokamana na kosa hili baya. Mwanamke haachiki kwa sababu ya kulaani. Anaendelea kubaki chini ya usimamizi wa mume wake.

[1] al-Bukhaariy (48) na Muslim (64).

[2] al-Bukhaariy (6105) na Muslim (110).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/398)
  • Imechapishwa: 25/07/2021