La kufanya pindi mji mzima hauna wanachuoni


s

Swali: Ikiwa mji wetu hauna wanachuoni wa kuwarejelea katika mambo ya Ijtihaad na Fataawaa za Kishari´ah tufanye nini?

Jibu: Sidhani kama kuna nchi yoyote katika ardhi ambayo haina wanachuoni na wanafunzi. Wapo angalau ni wachache. Sidhani kama nchi nzima itakosa kabisa mwanachuoni hata mmoja. Hili ni mosi.

Pili lau tutakadiria kuwa nchi mzima haina wanachuoni mawasiliano leo yamekuwa ni sahali; simu za ndani, simu za mkononi na barua pepe. Wasiliana na wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13974