La kufanya kwa mzee mwenye uzito wa kuswali kila swalah kwa wakati wake

Swali: Inajuzu kwa mwanamke mtumzima ambaye ana uzito wa kutia wudhuu´ kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr, Magrhrib na ´Ishaa? Je, inafaa kwake kufanya Tayammum?

Jibu: Ikiwa ana uzito wa kuswali basi hukumu yake ni kama ya mgonjwa. Hivyo ataruhusika kukusanya kati ya swalah mbili. Lakini hata hivyo asizifupishe. Bali ataswali Dhuhr Rak´ah nne na ´Aswr Rak´ah nne katika wakati mmoja. Kadhalika Maghrib Rak´ah tatu na ´Ishaa Rak´ah nne katika wakati mmoja, kama anavofanya mgonjwa.

Kuhusu kufanya Tayammum haifai kwake. Ni lazima kwake kutawadha na awe na mtu wa kumsaidia [kutia wudhuu´].

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 12/04/2019