Kuhusu kwenda sambamba na imamu ni jambo limechukizwa isipokuwa katika Takbiyrat-ul-Ihraam. Wanachuoni wametaja kwamba kwenda sambamba na imamu Takbiyrat-ul-Ihraam kunazuia kufungika kwa swalah na hivyo itamlazimu mswaliji kusubiri mpaka imamu amalize kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam. Baada ya hapo ndio na yeye aseme “Allaahu Akbar”. Wamesema kwamba akisema “Allaahu Akbar” kabla ya imamu kumaliza kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam, basi swalah yake haisihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (20) http://binothaimeen.net/content/6841
  • Imechapishwa: 25/09/2021