Kwenda miji ya makafiri kwa ajili ya masomo

Swali: Sisi ni vijana wa kiislamu ambao tunasoma USA kwa kipindi kati ya miezi sita mpaka miaka minne. Tulikuja kusoma hapa kwa khiyari yetu. Kwa msemo mwingine sio wenye kudhaminiwa kutoka upande wowote. Masomo hapa USA hayatofautiani na masomo katika miji yetu mbali na kufikia lugha ya kingereza. Ni ipi hukumu ya kukaa kwetu katika nchi hii kwa ajili ya masomo?

Jibu: Yule miongoni mwenu ambaye ana elimu na maarifa juu ya dini ya Allaah basi anaweza kulingania kwa Allaah, akawafunza watu kheri, akajizuilia shubuha dhidi ya nafsi yake na akadhihirisha dini yake kati ya wale makafiri anaoishi nao basi hakuna neno. Kwa sababu kukaa kwake kutokana na hali iliyotajwa na akajipatia elimu anayoihitaji ambayo itakuja kumfaa ni jambo lenye manufaa kwake na kwa wengine. Pengine Allaah akaongoza umati mkubwa kupitia kwake endapo atajipinda katika kulingania, akasubiri na akaitakasa nia yake kwa Allaah. Kuhusu ambaye hana elimu na maarifa, hana subira juu ya kulingania, anachelea juu ya nafsi yake kutumbukia katika yale aliyoharamisha Allaah, hawezi kuidhihirisha dini yake kwa kulingania katika kupwekeshwa Allaah na kutahadharisha shirki na akabainisha hayo kwa wale walioko pambizoni mwake basi haijuzu kwake kukaa kati ya washirikina. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi najitenga mbali na kila muislamu anayeishi kati ya washirikina.”

Jengine ni kutokana na ile khatari juu yake juu ya kuishi huku.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/401)
  • Imechapishwa: 26/07/2021