Kwenda miji ya makafiri kwa ajili ya masomo peke yake

Swali: Ni ipi hukumu ya kusafiri kwenda katika miji ya makafiri kwa ajili ya masomo?

Jibu: Kusafiri kwenda katika miji ya makafiri ni jambo la khatari ambalo ni lazima mtu ajihadhari nalo isipokuwa wakati wa dharurah kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mimi najitenga mbali na kila muislamu anayeishi kati ya washirikina.”

Hii ni khatari ambayo ni lazima kuihadhari. Ni lazima kwa nchi kutowatuma watu katika nchi za makafiri isipokuwa wakati wa dharurah. Sambamba na hilo ichunge wale inaowaagiza sio miongoni mwa wale wanaokhofiwa kutokana na elimu, utukufu na kumcha kwao Allaah. Wale wanaoagizwa wawe na watu wenye kuwachunga na kuziangalia hali zao. Vivyo hivyo ikiwa wale wajumbe wanasimama kwa kazi ya kulingania katika dini ya Allaah na kuenea Uislamu kati ya makafiri kutokana na elimu na utukufu wao. Jambo hilo linatakikana na hakuna neno.

Kuhusu kuwaagiza vijana katika miji ya makafiri kinyume na sura tuliyoitaja au kuwaruhusu kusafiri kwenda huko, ni uovu na kuna khatari ilio kubwa. Kadhalika wafanyabiashara kwenda huko kuna khatari kubwa. Kwa sababu nchi za kikafiri ushirikini na madhambi na maharibifu yako waziwazi. Mtu yuko khatarini kutokana na shaytwaan wake, matamanio yake na marafiki wabaya. Kwa ajili hiyo ni lazima kuhadhari na hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (07/295)
  • Imechapishwa: 13/06/2021