Kwenda kwa waganga pasi na kuwasadikisha?

Swali: Amekuja mtu na kunambia kuwa mke wangu amerogwa na kwamba hakuna ubaya kwenda kwa mganga lakini nisimsadikishe. Ni ipi hukumu ya jambo hilo?

Jibu: Hapana, usimsadikishe mchawi na wala usende kwa wachawi. Msomee Qur-aan na wakati wasoma wamtemea chache za mate na pia Aayat-ul-Kursiy, al-Faatihah, al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas na kwa hayo atapona – Allaah akitaka. Yeye pia mwanamke ajisomee mwenyewe na aseme:

أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

”Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia kutokamana na shari Alivyoviumba.”

na hivyo atapona – Allaah akitka. Pia asome al-Faatihah, Aayat-ul-Kursiy, al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas. Wewe msomee na yeye mwenyewe pia ajisomee. al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas azikariri kuzisoma mara tatu. Ni miongoni mwa sababu ya ponyo na kusalimika kutokamana na majanga yote. Haijuzu kwenda kwa wachawi, kuwauliza wala kuwasadikisha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3751/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%87%D8%A7%D8%A8-%D9%84%D9%84%D9%83%D8%A7%D9%87%D9%86-%D8%AF%D9%88%D9%86-%D8%AA%D8%B5%D8%AF%D9%8A%D9%82%D9%87
  • Imechapishwa: 18/05/2020