Kwenda kuswali msikiti wa mbali kwa ajili ya kupiga hatua zaidi?

Swali: Bora kwangu kuswali kwenye msikiti ulio karibu na nyumbani kwangu au msikiti ulio mbali zaidi na nyumbani kwangu kwa makusudio ya kupiga hatua zaidi kwenda msikitini?

Jibu: Hili linatokana kwa kutegemea watu. Ikiwa msikiti ulio karibu kuna athari kwa kuondoka kwako ambapo watu na imamu wanaanza kujiuliza umepotelea wapi, maamuma wanaanza kumtuhumu imamu na kuanza kusema fulani asingeenda kule kama hapa kuna kasoro na fulani akaacha kuswali nyuma yake. Ikiwa kunapelekea katika madhara basi swali katika msikiti wako wa karibu. Ama kukiwa hakuna madhara yoyote ni sawa ukaenda katika msikiti wa mbali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 08/04/2019