Swali: Mimi huenda kuswalia jenaza kila siku na kulisindikiza mpaka makaburini kulizika. Kuna mtu anayenikataza na kusema hili halikufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni kupetuka mipaka. Je, kunikataza kwake ni sahihi au kitendo changu mimi ndio sahihi?
Jibu: Kukukataza kwake sio sahihi. Kwa kuwa wewe unataka ujira na thawabu juu ya hilo. Unafanya vizuri. Hakuna neno. Kwa tendo lako hili unatarajiwa juu yako kupata thawabu – Allaah akitaka.
Lakini usijipe uzito. Ikiwa kuna uzito juu ya nafsi yako, usijitie uzito.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-10-29.mp3
- Imechapishwa: 11/11/2014