Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliekwenda jihaad bila wazazi kujuwa na akafariki -Allaah amrehemu – je, anaingia katika hukumu ya aliyepigana jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Tunataraji kwake jambo hilo – Allaah akitaka. Tunataraji amekufa hali ya kuwa ni shahidi na aliesameheka kwa kitendo, kwa sababu kwenda kwake pasi na idhini ya wazazi wake kunatokana na kujitahidi kwake na mapenzi yake juu ya kheri. Kuwaomba idhini wazazi wawili kuna tatizo [linaofanywa na wengi] kama mfano wa mtu huyu. Kwa hiyo tunataraji kwake kheri kubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4272/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B0%D9%87%D8%A8-%D9%84%D9%84%D8%AC%D9%87%D8%A7%D8%AF-%D8%AF%D9%88%D9%86-%D8%B9%D9%84%D9%85-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%AF%D9%8A%D9%87-%D9%88%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%B4%D9%87%D8%AFvidh
  • Imechapishwa: 12/06/2020