Swali 120: Je, inajuzu kutoka katika Jihaad pasi na idhini ya mtawala pamoja na kupatikana radhi za wazazi wawili?

Jibu: Kupigana Jihaad pamoja na nani? Ni kiongozi yupi huyo ambaye wewe unataka kupigana chini ya uongozi wake? Nchi zina mikataba kati yazo. Kwa hivyo ni lazima upate idhini ya kiongozi ya kwenda katika nchi hiyo. Masuala haya yana misingi yake. Sio mambo ya vurugu. Kwa hivyo mtawala akikupa idhini na mzazi wako akakupa idhini na wakati huohuo ukawa na uwezo basi hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 306
  • Imechapishwa: 27/10/2019