Kweli kwamba al-Albaaniy hakusoma chini ya wanachuoni?


Swali: Kuna utata unaenezwa kwamba Shaykh al-Albaaniy hakusoma kwenye mikono ya wanachuoni.

Jibu: Hili sio sahihi. Kauli inayosema kuwa Shaykh al-Albaani hakusoma kwa wanachuoni sio sahihi. Hili ni kosa. Uhakika wa mambo unamkadhibisha. Mwenye kusema haya amechukua maneno haya kutoka kwa yanayoenezwa na maadui wa Shaykh (Rahimahu Allaah). Si kweli. Kuna ambao wameandika juu ya hili na kuliradi na kuliangusha. Kitabu cha mwisho na pengine mkawa mmeshakisikia au wengi wenu mnakijua ni ndugu yetu Dr. Muhammad bin ´Umar Bazmuul. Amebainisha utata huu na kuuangusha katika kitabu chake “Sharh Swifat as-Swalat an-Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)” na amebainisha waliimu wa Shaykh. Miongoni mwa waalimu zake wa mwanzo ni baba yake. Baba yake alikuwa ni mwanachuoni wa Fiqh katika wanachuoni wa Hanafiyyah. Alikuwa amebobea Fiqh ya Hanafiy. Alijifunza kwake. Rejeeni kwa kitabu cha Dr. Muhammad bin ´Umar Bazmuul. Allaah Amjaze kheri. Aliyoandika ni bayana yenye kutosheleza na ya mukhtasari.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin ´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net
  • Imechapishwa: 07/05/2018