Kwanini wasikufurishwe Suufiyyah wenye kuonelea Wahdat-ul-Wujuud na Huluul?

Swali: Suufiyyah wenye kuonelea nadharia ya kwamba viumbe vyote ni Allaah (Wahdat-ul-Wujuud) na kwamba Allaah amekita na kuchanganyika kwenye kila kitu (Huluul) wanakufuru au ni lazima kwanza wasimamishiwe hoja?

Jibu: Ndio, wanakufuru. Wamefikiwa na hoja. Kuna uwezekano wakawa hata wamehifadhi Qur-aan na katika wao kukawepo wasomi wa Hadiyth ambao wamehifadhi vitabu vya “as-Swahiyh”. Hoja imewasimamia.

 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 16/11/2016