Mtu asitamani kupona na akachukulia sahali masuala haya. Akaenda kuchukua (dawa) kwa wachawi na akachukua nasaha zao. Wakamfanyisha Shirki na kufanya Shirki na akamshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla) kwa madai ya kutamani kupona kwa maradhi. Na wanaweza wakasema baadhi yao ya kuwa hii ni dharurah. Hii sio dharurah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Hakufanya dawa yetu kwa yale Aliyotuharamishia. Hii sio dharurah. Kwa kuwa Allaah Hakufanya dawa ikawa katika Haramu. Hakufanya dawa katika Haramu, vipi tusemeje kuhusu Shirki? Hakuna dharurah. Allaah Kawawekea Waislamu Ruqyah ya Kishari´ah, Ruqyah yenye kunufaisha na Ruqyah yenye manufaa. Ni juu yao waishie katika Aliyoweka Allaah na ndani yake kuna kheri nyingi. Na lau wangelitumia Aliyoruhusu na Kuweka Allaah na huku wakamuamini Allaah, basi Allaah Angeliwafaa kwa hilo na dawa ingelipatikana kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=s_rSMq7OiHE
  • Imechapishwa: 23/03/2018