Kwanini unababaika, kuongeza mke ni haki yako?


Swali: Mke wangu ananishakia kuwa nitaoa mke mwingine na mimi nanuia hilo huko mbeleni. Je, inajuzu kwangu ili kujiepusha na khatari yake, yaani kwa kumwambia “Mke wangu, nikioa mwanamke mwingine asiyekuwa wewe nitakuwa nimemtaliki”?

Jibu: Wewe ndugu! Kwa nini ujifiche? Ukioa, Alhamdulillaah. Ikiwa umekamilisha sharti ya uadilifu, oa na si lazima umshauri kwanza. Hii ni haki yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/10045
  • Imechapishwa: 01/03/2018