Kwanini Damu Ndogo Inasamehewa Lakini Si Mkojo?


Swali: Kwa nini wanachuoni wamesema kuwa damu ndogo ikiingia kwenye nguo ndani ya swalah inasamehewa lakini mkojo mdogo hausamehewi?

Jibu: Kwa sababu kuhusiana na damu kuna tofauti kama ni najisi au si najisi. Tofauti na mkojo kuna maafikiano kuwa ni najisi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt--14340506.mp3
  • Imechapishwa: 07/04/2017