Kwanini asikufurishwe mwenye kusema kuwa Sunnah haiendani na wakati wa leo?

Swali: Baadhi ya watu wanapoamrishwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama mfano wa ndevu na kanzu, wanasema haya hayaendani na wakati wa leo, kwamba yeye anaogopa asikose mtu wa kumuozesha au kutuhumiwa kwamba ni gaidi. Ni ipi hukumu ya hali hizi? Je, kunazingatiwa ni kuritadi?

Jibu: Hali ya kwanza akisema kwamba hayaendani na wakati wa leo kunazingatiwa ni kuritadi. Ama hali ya pili akisema kwamba anaogopa asije kuozwa na mfano wa hayo. Haihesabiki ni kuritadi. Lakini inahesabika ni upotevu na makosa. Kwa sababu ameacha kwa sababu ya kuwaogopa watu. Inahusiana na yule ambaye hasemi kuwa hayaendani na wakati wa sasa. Anasema kuwa yanaendana na wakati wa leo. Lakini anakhofia asije kuozeshwa, watu wakamcheka na mfano wa hayo. Huu ni upotevu na makosa na sio kuritadi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
  • Imechapishwa: 17/11/2018