Kwanini asikufurishwe asiyeamini kuwa watu watafufuliwa?

Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunaamini kufufuliwa, matendo kulipwa siku ya Qiyaamah, kiwanja, hesabu, kusoma madaftari, thawabu, adhabu, Njia (Swiraat) na mizani.”

Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kuamini kufufuliwa, miili kurudishwa, matendo kulipwa, kiwanja na hesabu, kusoma madaftari, thawabu na adhabu, Njia na mizani. Asiyeamini kuwa Allaah ataifufua miili na kuzirusha roho ni kafiri kwa maafikiano ya waislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/636)
  • Imechapishwa: 19/05/2020