Kwanini asikufurishwe anayepinga kuwepo kwa wanawake wa Peponi?

Swali: Kuhusiana na imani ya kuamini siku ya Mwisho ni lazima kwa mtu kuamini ufafanuzi wake wote? Kuna mtu anayeamini siku ya Mwisho, lakini anakanusha kuwepo kwa al-Huur al-´Ayn na anasema kuwa Aayah zilizothibiti juu yake makusudio yake ni ladha na neema atakazopata muumini Peponi…

Jibu: Mwenye kupinga kitu miongoni mwa mambo ya Aakhirah, ni mamoja cha Pepo au Moto, au akakiwekea tafsiri mbovu kinyume na maana yake sahihi, ni kafiri.

Qur-aan haifasiriwi kwa maoni au ufikiriaji. Qur-aan inafasiriwa kwa njia zake sahihi zilizowekwa. Qur-aan inafasiriwa kwa Qur-aan, Sunnah, kwa tafsiri ya Maswahabah na Taabi´uun au kwa lugha yake. Qur-aan haifasiriwi kwa fikira au maoni. Mwenye kuzungumza juu ya Qur-aan kwa maoni yake na kwa yale asiyoyajua, ajiandalie makazi yake Motoni – amekosea hata kama atapatia. Qur-aan haifasiriwi isipokuwa kwa njia zake zinazojulikana. Si kila mtu anastahiki kufasiri Qur-aan kwa matamanio yake na uelewa wake. Baya zaidi kuliko hili ni pale ambapo atakanusha baadhi ya yaliyomo kwenye Qur-aan na akayapinga na akayawekea tafsiri mbovu kinyume na maana yake ilokusudiwa na akazungumza juu ya Allaah pasi na elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (53) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-25_0.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020