Kwanini asikufurishwe anayepinga Israa´ na Mi´raaj?


Amesema (Ta´ala):

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ

“Utakasifu ni wa ambaye Amemsafirisha mja Wake usiku kutoka al-Masjid al-Haraam kwenda al-Masjid al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake.” (17:01)

Yule mwenye kupinga Israa´ anakufuru kwa kuwa ni mwenye kumkadhibisha Allaah.

Mi´raaj [kule kupandishwa mbinguni] vilevile imethibiti katika Hadiyth Swahiyh ambazo zinafidisha elimu yenye kukata mashauri kabisa. Hata hivyo yule mwenye kupinga hili hakufurishwi mpaka asimamishiwe kwanza hoja na kuwekewa wazi.

Asli ya maana ya Israa´ kilugha ni kusafiri usiku.

Israa´ Kishari´ah na kiistilahi ni safari ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka Makkah kwenda Yerusalemu usiku akiwa juu ya mpando al-Buraaq.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/292)
  • Imechapishwa: 21/05/2020