Swali: Katika moja ya nchi za UAE amejitokeza bwana mmoja anayedai kuwa yeye ndiye al-Mahdiy anayesubiriwa kisha hivi sasa amedai kuwa ni Mtume. Bwana huyu ana wafuasi wengi ambao wanamwamini kufikia kiasi cha yakini. Ni ipi hukumu ya bwana huyu na wafuasi wake?

Jibu: Bwana huyu ambaye muulizaji anasema kuwa andai kuwa ndiye al-Mahdiyh mtarajiwa kisha akadai kuwa ni Mtume na kwamba ana wafuasi, bwana huyu ni moja ya mambo mawili: ima ana kasoro akilini mwake. Ikiwa ana kasoro akilini mwake basi itambulike kuwa kalamu yake imenyanyuliwa.

Ama ikiwa akili zake ni timamu, kama yuko katika nchi yetu basi ni lazima kwenda kumshtaki mahakamani na auwawe. Kwa sababu anastahiki kuuawa. Ikithibiti kweli kwamba anadai kuwa ni Mtume basi anapaswa kusimamishiwa adhabu na kuuawa. Hili ndio jambo linalotakikana. Kuhusu masuala ya kumjibu hakuna haja ya kumjibu wala haimnufaishi kitu Radd. Hakuna kinachomstahikia mtu huyo isipokuwa kumsimamishia adhabu ya Kishari´ah. Akiwa ni mwenye akili timamu… ni lazima kwa muulizaji na wengineo wathibitishe jambo hili na waende kumshtaki mahakamani, wamlete na wahakikishe jambo lake. Ikithibiti kuwa kweli amedai kuwa ni Mtume nasi anauawa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/49/%D8%B1%D8%AC%D9%84-%D9%8A%D8%AF%D8%B9%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%87%D8%AF%D9%8A%D8%A9-%D8%AB%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%88%D8%A9
  • Imechapishwa: 16/01/2020