Swali: Kuna mtu ni muislamu kwa baba na mama lakini hata hivyo amekataa swalah, swawm na mambo mengine katika Shari´ah ya Allaah. Je, inajuzu kutangamana naye matangamano ya waislamu kwa mfano muislamu kula pamoja naye na mengineyo?

Jibu: Hali ya mtu huyu ikiwa ni hii uliyotaja, ya kukataa swalah, swawm na mambo mengine ya Shari´ah ya Uislamu, ni kafiri kufuru yenye kumtoa katika Uislamu kutokana na kauli sahihi katika kauli za wanachuoni. Anatakiwa kuambiwa kutubia kwa siku tatu, akitubu ni sawa, la sivyo mtawala wa waislamu amuue kama wanavyouawa wenye kuritadi.

Haijuzu kwa waislamu kumpenda, kumtembelea na kadhalika. Isipokuwa ikiwa kama itakuwa ni kwa lengo la kumnasihi na kumwelekeza na kumuadhisha. Huenda akatubu kwa Allaah (Subhaanah).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/32)
  • Imechapishwa: 24/08/2020