Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye ameingia katika Uislamu punde tu akiomba uokozi kutoka kwa asiyekuwa Allaah au akaomba maiti pamoja na kujua kwamba anaishi mbali na wanachuoni?

Jibu: Ni mshirikina kwa kuwa amefanya shirki. Huyu ni mshirikina kwa kuwa amemfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah. Lakini ni mwenye kupewa udhuru au si mwenye kupewa udhuru? Ikiwa hakusikia kuhusu Uislamu na wala hakujua basi atambue kuwa Allaah amesema:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

“Hatukuwa ni wenye kuadhibu mpaka Tupeleke Mtume.” (17:15)

Siku ya Qiyaamah atapewa mtihani. Kuna maandiko yamekuja kuonyesha kuwa wale ambao hawakufikia na Ujumbe watapewa mtihani.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/AudioDir2/67848.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2017