as-Suwaydaan amesema: “Mimi hata hadd [adhabu] ya kuritadi sioni kama ni ya kidini. Naona ni kama adhabu ya kisiasa tu.”

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema adhabu ya kuritadi ni ya kisiasa na sio ya kidini akitumia hoja kwa Kauli Yake (Ta´ala):

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika dini.”? (02:256)

Jibu: Adhabu ya kuritadi imethibiti kwa maafikiano na Hadiyth Swahiyh. Maneno ya watu hawa hayaathiri kitu. Wanachuoni wamekubaliana juu ya hili. Aayah:

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika dini.”

inahusiana na kuingia katika dini. Hakuna mwenye kutenzwa nguvu kuingia katika Uislamu. Kuingia ni kwa khiyari. Lakini yule mwenye kuingia na akakiri kuwa ni haki kisha baadaye akaiacha dini, anaihujumu na kuiharibu ´Aqiydah. Kuna khatari wengine wakamuiga baada yake. Ndio maana ni wajibu kumuua:

وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Na kundi miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab likasema: “Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini [yaaminini] mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea.” (03:72)

Bi maana ili wawaigeni na wauache Uislamu. Anayesema kuwa murtadi asisimamishiwe adhabu na kwamba ni jambo la kisiasa na ni kama mayahudi na manaswara. Ni jambo la kidini na sio la kisiasa. Adhabu inailinda ´Aqiydah. Ulinzi wa ´Aqiydah ni moja katika mambo ya kidharurah matano na jambo la kwanza la kidharurah ni kuilinda ´Aqiydah isije kuchezewa na upumbavu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 24/05/2018