Swali: Umesema kuwa mwenye kuhukumu kwa kanuni za kutungwa ni kafiri. Kunaenezwa uvumi ya kwamba umejirejea. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Mimi sina haki ya kurejea kama ambavyo pia sina haki ya kukufurisha isipokuwa kwa Qur-aan na Sunnah. Yule mwenye kuhukumu kwa kanuni za kutungwa na wakati huohuo anaonelea kuwa ni bora kuliko, anaona kuwa zinalingana na Qur-aan na Shari´ah au anaona kuwa ana khiyari; huyu hakuna shaka yoyote juu ya ukafiri wake kwa mujibu wa wanachuoni wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13958
  • Imechapishwa: 24/06/2020