Swali: Ni ipi hukumu ya maamuma kuzungumza ndani ya Swalah ikiwa kuzungumza huku kuna maslahi ya Swalah kwa mfano kusema kumwambia Imamu “Zidisha Rakaa moja”?
Jibu: Hapana, haijuzu. Swalah inabatilika. Kuleta maneno kwa kukusudia kunabatilisha Swalah.
وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ |
“Na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.” (02:238) |
Tumeamrishwa kunyamaza na tumekatazwa kuleta maneno. Badala ya kuzungumza aseme “Subhaana Allaah”.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-04-08.mp3
- Imechapishwa: 16/11/2014