Swali: Ni ipi hukumu ya maamuma kuzungumza ndani ya swalah ikiwa kuzungumza huku kuna maslahi ya swalah kwa mfano kusema kumwambia imamu “Zidisha Rak´ah moja”?

Jibu: Hapana, haijuzu. Swalah inabatilika. Kuleta maneno kwa kukusudia kunabatilisha swalah.

وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

“Simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.” (02:238)

Tumeamrishwa kunyamaza na tumekatazwa kuleta maneno. Badala ya kuzungumza aseme “Subhaana Allaah”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-08.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014