Kuzungumza baada ya Iqaamah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzungumza baada ya kukimiwa swalah na kabla ya Takbiyrat-ul-Ihraam juu ya mambo yasiyohusiana na swalah kama kusawazisha safu na mengineyo au maneno yakahusiana na maisha ya kidunia?

Jibu: Kuzungumza baada ya kukimiwa swalah na kabla ya kuanza kuswali ikiwa yanahusiana na swalah kama mfano wa kusawazisha swalah na mfano wake ni kitu kinakubalika katika Shari´ah. Na kama hayahusiani na swalah basi bora ni kuacha kufanya hivo kwa ajili ya kujiandaa kuingia ndani ya swalah na kuitukuza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/358)
  • Imechapishwa: 20/09/2021