Kuzindukana wakati adhaana imefika katikati

Swali: Mtu afanye nini lau muadhini ataadhini ilihali mtu ameghafilika na akaja kuzindukana wakati ambapo adhaana imefika mwisho? Je, aanze mwanzo kisha aendelee kumuitikia au tuseme kuwa ni Sunnah iliyopita mahala pake?

Jibu: Amuitikie sehemu iliyobaki. Muadhini akimaliza alete kile kilichompita na kuomba du´aa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (66) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020