Kuzichanua nywele na kuzilaza upande mmoja

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchanua nywele za kuzilaza au ni haramu?

Jibu: Kuchanua kwa kuzilaza ni kitu ambacho sikioni. Lakini ikiwa anachokusudia ni kuzichanua kwa kuzilaza upande mmoja basi atambue kuwa kufanya hivo ni kwenda kinyume na Sunnah. Sunnah ni kuzitengeneza kichwani kutokea katikati ili nywele zitandae pande zote mbili na ziwe sawasawa upande wa kulia na upande wa kushoto.  Hiki ndicho anachotakiwa mwanamke kufanya. Ama akizichanua upande mmoja ni kitu kisichotakiwa na khaswakhaswa ikiwa amekusudia kujifananisha na wasiokuwa waislamu, hapo itakuwa haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6805
  • Imechapishwa: 07/03/2021