Kuzembea baada ya Ramadhaan si dalili ya kutokukubaliwa


Swali: Kuzembea juu ya matendo mema baada ya Ramadhaan ni dalili inayofahamisha kutokukubaliwa? Mimi nahisi kuzembea na nachelea Allaah asiwe amenikubalia?

Jibu: Hii sio dalili kwamba Allaah hakupokea kutoka kwako. Lakini hata hivyo ni dalili ya udhaifu wa hima na kutokuwa na khofu. Kwa ajili hiyo mtu anatakiwa aisubirishe nafsi yake na aivumilishe juu ya matendo mema. Kwa sababu kwa kweli Ramadhaan ni masomo. Siku thelathini au ishirini na tisa zinapita na wewe umeshughulishwa na kufanya ´ibaadah mbalimbali. Kwa hiyo ni lazima yauathiri moyo wako na mwenendo wako. Kwa hiyo tumia fursa hii.

Ama kusema kwamba yule mwenye kurudi katika madhambi baada ya Ramadhaan ni dalili inayoonyesha kutokukubaliwa, hatuwezi kusema hivi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/930
  • Imechapishwa: 07/05/2018