Swali: Ni ipi hukumu kwa wanawake kuyatembelea makaburi kama mama kumtembelea mtoto wake?

Jibu: Haijuzu kwa wanawake kuyatembelea makaburi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi, wenye kuyafanya ni sehemu ya kuswalia na wenye kuyatia mataa.”

Matembezi yanakuwa kwa wanaume. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nilikuwa nimekukatazeni kuyatembelea makaburi. Hivi sasa yatembeleeni. Hakika yanakukumbusheni Aakhirah.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=63284&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 26/08/2017